Posts

KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO

Image
KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO Na Mwandishi wetu, NCAA. Hamasa ya  wananchi wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro  imeongezeka ambapo leo tarehe 19 February , 2024 jumla ya kaya 82 zenye wananchi 541 na mifugo 3,379 zimehama kutoka Ngorongoro kweda Kijiji cha Msomera Handeni Tanga. Akizungumza wakati wa kuaga kundi hilo Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Richard Kiiza amesema kuwa baada ya kuhama kwa kundi hilo leo inafanya idadi ya wananchi waliokwishahama ndani ya hifadhi tangu zoezi lilipoanza hadi leo kufikia kaya 1,032 zenye watu 6,395 na mifugo 28,982. Kamishna Kiiza amebainisha kuwa kadri siku zinavyoenda wananchi wengi wanahamasika na kujiandikisha kuhama kwa hiari yao wenyewe hasa baada ya ushuhuda wa maisha mazuri kwa wananchi wenzao waliokwishatangulia ambao Maisha yao yamebadilika kwa kiasi kikubwa. “Wananchi waliotangulia mwaka jana wengi wao wamejenga nyumba za kisasa, wamelima mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na ...

UTALII WA MALIKALE WASHIKA KASI NCHINI, WAFARANSA WAFURIKA KILWA KISIWANI

Image
UTALII WA MALIKALE WASHIKA KASI NCHINI,  WAFARANSA WAFURIKA KILWA KISIWANI   Na Beatus Maganja Kwa miongo kadhaa kumekuwa na dhana ya kwamba wageni wengi wa nje hupendelea zaidi utalii wa kuona wanyamapori, lakini hivi karibuni dhana hiyo imeanza kubadilika kwa kasi ambapo Tanzania imeanza kupokea wageni makundi kwa makundi wakitembelea katika maeneo yetu ya Malikale hususan Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara. Ni takrikani siku 9 sasa katika kipindi cha Mwezi Februari kuanzia tarehe 03 - 11, 2024, Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imeweza kushuhudia   Meli zilizosheheni makundi ya Watalii kutoka Mataifa mbalimbali zikipishana kutia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara na kufikisha idadi ya watalii wapatao 445 kwa safari nne (4) za kitalii zilizofanyika. Kwa mara nyingine Februari 11, 2024 TAWA ilipokea kundi la nne (4) la watalii wapatao 114  kutoka Ufa...

RAIS SAMIA ARIDHIA KUANZISHWA KWA MTAALA WA MASOMO YA UTALII

Image
RAIS SAMIA ARIDHIA KUANZISHWA KWA MTAALA WA MASOMO YA UTALII Na Happiness Shayo-Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuanzishwa kwa masomo ya Utalii kwa kidato cha tano na sita nchini lengo ikiwa ni kuendelea kuikuza Sekta ya Utalii. Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao kati yake na Wabunge wa Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kilichofanyika ukumbi wa Utawala Bungeni jijini Dodoma leo. “Tunashukuru Mheshimiwa Rais aliona umuhimu wa kuanzishwa kwa mchepuo wa masomo ya utalii na hakuchukua muda mrefu kulikubali suala hilo” Mhe. Kairuki amesisitiza. Amesema lengo la kuanzishwa kwa mchepuo wa masomo ya utalii ni kuendelea kuiboresha sekta hiyo akitolea mfano kutoa mafunzo ya utoaji wa huduma kwa wateja, lugha na kadhalika. Amesema ameshawasilisha toolkit ya mchepuo huo  ambayo inaendana na matakwa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani ( World Tourism Organization-UNWTO)pamoja n...

MELI YENYE WATALII ZAIDI YA 100 YATIA NANGA HIFADHI YA MAGOFU YA KALE KILWA KISIWANI

Image
  MELI YENYE WATALII ZAIDI YA 100 YATIA NANGA HIFADHI YA MAGOFU YA KALE  KILWA KISIWANI Na mwandishi wetu/Kilwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Februari 03, 2024 imepokea meli kubwa ya watalii wapatao 102 kutoka uingereza waliofika katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya shughuli za utalii kisiwani humo. Watalii hao wakiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Takim Holidays walipokelewa na kukaribishwa kwa ngoma za asili ya watu wa Kilwa Kisiwani iitwayo kitupolo ambayo iliwafanya waonekane wakifurahi muda wote. Ngome ya Mreno, Msikiti mkubwa na mkongwe, Makaburi ya Malindi na Makutani Palace ni miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na watalii hao ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kujifunza tamaduni za watu wa Kilwa kisiwani. Historia na upekee wa Hifadhi hii ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka Kona mbalimbali za Dunia ambao hutembelea Hifadhi hiyo Karibu Kila Mwa...

SHIRIKA LA CTG - CHINA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTANGAZA UTALII

Image
SHIRIKA LA CTG - CHINA  KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTANGAZA UTALII  Na Happiness Shayo Shirika la Kiserikali la China linalosimamia utangazaji wautalii  na uwekezaji  (China Tourism Group - CTG) limeonesha nia ya kutaka kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania pamoja na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya Sekta ya Utalii nchini kwa  lengo la  kukuza utalii wa Tanzania na kuongeza mapato yatokanayo na Sekta hiyo. Hayo yamesemwa leo Februari 1,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao kati ya shirika hilo pamoja na Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kilichofanyika Jijini Dodoma. Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki amesema  Tanzania itanufaika na ushirikiano huo ambapo moja ya kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuvutia watalii wengi kutoka nchi za nje hivyo, Serikali itatumia fursa hiyo kuvutia watalii kutoka soko la China. Aidha, Mhe. Kairuki ameliomba  Shirika hilo kuwekeza kati...

MWAROBAINI WA MIUNDOMBINU KOROFI SERENGETI WAPATIKANA

Image
  MWAROBAINI WA MIUNDOMBINU KOROFI SERENGETI WAPATIKANA      Na. Edmund Salaho/Serengeti. Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA Juma Kuji leo amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kushughulikia mara moja maeneo korofi ya barabara ndani ya hifadhi hiyo, ili watalii wafikie adhma yao ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti. Akizungumza baada ya kukagua maeneo hayo Kamishna Kuji, ameielekeza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kurekebisha maeneo yote korofi na kuhakikisha kuwa hakuna maeneo ambayo hayatapitika licha ya uwepo wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ili kupunguza adha kwa wageni. “Licha ya changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea hatuwezi kusubiri ziishe tumeazimia kushughulikia kwa haraka maeneo yote korofi ikiwa ni hatua za haraka, lakini lengo kuu ni kuhakikisha  barabara hizi zinakuwa na tabaka gumu, haya ni maagizo yangu kwa menejimenti kuhakikisha barabara zote zi...

TTB NA TANAPA WATANGAZA UTALII WA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA FITUR - MADRID

Image
TTB NA TANAPA WATANGAZA UTALII WA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA FITUR - MADRID   Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake za TANAPA  na TTB wanashiriki Onesho la Fitur - Madrid Hispania kwa lengo la kunadi na kuhamasisha watalii wengi zaidi kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania. Onesho hilo linatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 220,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani. Katika Onesho hilo pia TANAPA inaendelea kunadi fursa za uwekezaji zinazopatikana  ndani ya hifadhi hizo. Aidha, onesho hilo mbali na kuwashirikisha TTB na TANAPA pia limewajumuisha wadau wa utalii na limeanza tarehe 24.01.2024 na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 28.01.2024 .

HAKUNA MWANANCHI WA NGORONGORO ATAKAYEKOSA HAKI YAKE-RC MONGELLA

Image
 HAKUNA MWANANCHI WA NGORONGORO ATAKAYEKOSA HAKI YAKE-RC MONGELLA  Na mwandishi Wetu, NCAA Mkuu wa Mkoa wa Arusha mheshimiwa John Mongella amewahakikishia wananchi wanaohama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi  kuwa serikali imejipanga na hakuna mwananchi yoyote atakayekosa haki zake iwapo ataamua kuhama kwa hiyari. Mheshimiwa Mongella ametoa kauli hiyo wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha leo tarehe 25 Januari, 2024 wakati akiwaaga wananchi 818 walioamua kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kwenda kuishi katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga. Ameeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa na  hakuna mwananchi yoyote atakayekosa kulipwa haki zake zote zilizoanishiwa katika utekelezaji wa zoezi hilo. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa zoezi hilo linatekelezwa kwa kuzingatia misingi yote...
Image
  TAWIRI  NA MUENDELEZO WA TAFITI UGONJWA WA TWIGA ULIOATHIRI ASILIMIA 62 YA TWIGA KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUAHA Na Mwandishi wetu, Arusha Taasisi ya Utafiti wa  Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) inaendelea kufanya  tafiti zaidi juu ya madhara na matibabu ya ugonjwa wa ngozi wa Twiga ambao  matokeo ya awali yameonyesha maeneo yanayoathirika ya viungio kwenye miguu (magoti) hususan miguu ya mbele, kuna vimelea vya bakteria, virusi na fangasi. Akizungumza wakati wa ufuatiliaji wa matibabu ya ugonjwa huo katika hifadhi ya Taifa Ruaha, Dkt. Julius Keyyu ambaye ni  Mkurugenzi wa Utafiti  TAWIRI,  amesema ugonjwa wa ngozi wa Twiga uliogundulika katika hifadhi  ya Taifa  Ruaha mwaka 2000 ni tofauti na ugonjwa wa ngozi wa Twiga katika nchi nyingine duniani  " tumefuatilia ugonjwa huu kwa nchi nyingine duniani na kubaini upo tofauti na hapa nchini" amebainisha  Dkt. Keyyu Dkt.Keyyu amesema asilimia  62% ya Twiga waliopo hifadhi ya ...
Image
MAKAMU WA RAIS WA CUBA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 - 25 Januari, 2024.  Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb.) Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere. Mhe. Mesa pia atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.