WAZIRI CHANA AFUNGUA RAS ONESHO LA WIKI YA UBUNIFU LA ITALIA JIJINI DAR ES SALAAM
• Aipongeza Italia kwa mashirikiano katika sekta ya utalii Na Happiness Shayo- Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefungua rasmi Onesho la Wiki ya Wabunifu wa Italia linaloonesha picha za wabunifu mbalimbali wakubwa wa zamani kutoka nchini Italia na kuipongeza nchi hiyo kwa ushirikiano kati yake na Tanzania kwenye sekta ya utalii. Ufunguzi huo umefanyika leo Februari 10,2025 katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam ambapo onesho hilo linatarajiwa kumalizika Februari 20,2025 likiwa na lengo la kukuza ushirikiano katika masuala ya utalii, historia na uchumi. “ Italia imejitolea katika juhudi zetu za kukuza utalii endelevu na kuhifadhi urithi wetu wa asili na kiutamaduni .Mfano mmoja mzuri wa ushirikiano huu ni mradi wa Kisiwa cha Bawe, ambao ni mwanzo mzuri unaoonyesha utalii endelevu. Mradi huu hauangazii tu uzuri wa visiwa vya Tanzania bali pia unaonesha matokeo chanya ya uwekezaji wa ki...